Wednesday, September 14, 2011

Serikali yatangaza mikoa mipya

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

TAARIFA KWA UMMA

NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Katika kutekeleza Mamlaka hayo, Rais ametoa notisi ya kusudio la kuanzisha Mikoa minne (4) na Wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002 ni Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa na Tangazo la Serikali Na. 287 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Wilaya.

Madhumuni ya Notisi hizi ni kuzialika Taasisi na mtu mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa Mikoa mipya na siku 30 kwa Wilaya mpya kuanzia tarehe ya Notisi hizi.

Baada ya muda uliowekwa kupita, Rais atachambua maoni, mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha rasmi Mikoa na Wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.

Mikoa mipya inayoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

MKOA WILAYA ZAKE MKOA ZINAKOTOKA MAKAO MAKUU
1. Geita Geita Mwanza Geita
Nyang’hwale(Mpya) Mwanza
Chato Kagera
Bukombe Shinyanga
Mpya/Mbogwe Shinyanga

2. Simiyu Bariadi Shinyanga Bariadi
Itilima (Mpya) Shinyanga
Maswa Shinyanga
Meatu Shinyanga
Busega (Mpya) Mwanza

3. Njombe Njombe Iringa Njombe
Wanging’ombe(Mpya) Iringa
Ludewa Iringa
Makete Iringa

4. Katavi Mpanda Rukwa Mpanda
Mlele(Mpya) Rukwa

Wilaya mpya zinazoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

WILAYA MPYA WILAYA MAMA MKOA MAKAO MAKUU
1. Buhigwe Kasulu Kigoma Buhigwe
2. Busega Magu Mwanza Igalukilo
3. Butiama Musoma Mara Nyamisisi
4. Chemba Kondoa Dodoma Chemba
5. Gairo Kilosa Morogoro Gairo
6. Ikungi Singida Singida Ikungi
7. Itilima Bariadi Shinyanga Itilima
8. Kakonko Kibondo Kigoma Kakonko
9. Kalambo Sumbwanga Rukwa Kalambo
10. Kaliua Urambo Tabora Kalua
11. Kyerwa Karagwe Kagera Rubwera
12. Mbogwe Bukombe Shinyanga Mbogwe
13. Mkalama Iramba Singida Nduguti
14. Mlele Mpanda Rukwa Inyonga
15. Momba Mbozi Mbeya Ndalambo
16 Nyang’hwale Geita Mwanza Nyang’hwale
17. Nyasa Mbinga Ruvuma Mbamba Bay
18. Uvinza Kigoma Kigoma Lugufu
19. Wanging’ombe Njombe Iringa Waging’ombe

Kwa taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya Taifa kwa ujumla. Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -


Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.

E-mail hakattanga@yahoo.com
Fax- 026-2322116


Imetolewa na: -

Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

9 Septemba, 2011

No comments: