Sunday, August 9, 2015

JE KUNA MGAWANYIKO NDANI YA JESHI LA POLISI?


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF HOME AFFAIRS TANZANIA POLICE FORCE Mheshimiwa Jakaya M. Kikwete Tar 6/08/2015 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Ikulu – Dar es salaam. Afande, Mheshimiwa Rais, YAH:- IGP ERNEST MANGU KUANDAA MPANGO WA KUVURUGA UCHAGUZI MKUU 2015 NA KUSIMAMIA HARAKATI ZA MPANGO WA UHAINI KWA KUSHIRIKI KUANDAA MAANDAMANO NA VURUGU ZA KUIONDOA SERIKALI HALALI MARA BAADA YA UCHAGUZI Mheshimiwa Rais, tafadhali tunaomba urejee somo husika hapo juu, Pamoja na kwamba tunajua umezongwa na mambo mengi, tunapenda ufahamu kwamba hali ndani ya Jeshi letu ni mbaya, na kila mmoja wetu anajua wazi kwamba ulipotoshwa mpaka ukafanya maamuzi ya kumteua IGP Ernest J. Mangu, mtu asiyekuwa na uwezo wa kiutendaji wala sifa za uongozi, uadilifu na uzalendo kushika wadhifa huu muhimu. Mheshimiwa Rais, tunajua waliokudanganya walikuwa na malengo yao. Ambayo mengine kwa macho yako umeyaona/unayaona na mengine utaendelea kuyathibitisha kwa kile kinachoendelea na yanayolengwa kutokea hapo mbele endapo hutachukua hatua za maamuzi ya kumwondoa mapema. Pia, tunaomba uelewe kwamba tunakuandikia barua hii ili kukujulisha mambo machache kuhusu mkakati wake na ‘washirika wake wa kisiasa’ wa kulivuruga Jeshi la Polisi. Wanafanya hivyo ili kufanikisha mpango wa kuvuruga uchaguzi mkuu ujao na kisha kulazimisha uwepo wa Serikali ya mseto kwa mtindo wa nguvu ya umma endapo wadau wake watakuwa wameshindwa. Katika kuhakikisha anafanikisha mikakati hiyo amekwishafanikiwa kutekeleza mambo mengi, baadhi ya mambo hayo ni haya yafuatayo:- (1) Kuhamisha na kupanga maRPC, RCO, SOI, OCD (katika mikoa lengwa) ambao watawezesha kukamilisha anayoyataka katika mikoa na maeneo lengwa. Na mahala pengine anafanya hivyo katika muda huu wa lala salama, ili kuwavuruga makamanda na maofisa tajwa ili wakati mchakato wa uchaguzi unafanyika wawe bado na ugeni wa kuyasoma na kuyaelewa mazingira mapya ya himaya za majukumu yao. (2) Kuhamisha dawati la kuratibu uchaguzi kutoka katika kamisheni ya oparesheni na kulipeleka kamisheni ya polisi jamii. Uamuzi huu hakuufanya kimakosa, alikusudia. Ndiyo maana kila anaposhauliwa kulirejesha panapostahili anakataa. Mheshimiwa Rais, katika hili tunaomba uelewe kwamba kulingana na muundo wa sasa wa Jeshi letu, mwenye jukumu la kuliandaa Jeshi kwa ajili ya uchaguzi na kusimamia askari katika oparesheni ya kufanikisha uchaguzi ni kamisheni ya oparesheni, lakini kwa kuwa anajua CP. Paul Chagonja hawezi kumpenyezea ‘upuuzi wa uasi’ wake na kwa kuwa anajua huyu CP anao uwezo, uzoefu na anajua mambo yanavyopaswa kufanywa katika wakati huu, amehamisha dawati hilo na kulipeleka katika kamisheni isiyohusika kabisa na anatumia fursa hiyo kuthibiti mambo muhimu yanayopaswa kufanyika kama sehemu ya maandalizi ya kufanikisha uchaguzi mkuu. Kwa sababu ya hali hiyo, mpaka sasa hakuna maandalizi ya maana yanayoendelea. Kinachofanywa ni udanganyifu na ubabaishaji ili ‘kuwazuga’ ninyi viongozi. Sisi tunaamini kwamba, mazingira ya kijamii na kisiasa yamebadilika na yataendelea kubadilika. Hivyo kwa wakati huu tulipaswa kuwa katika hatua ya pili ya maandalizi ili kujenga utayari na mifumo ya kuzuia na si kusubiri wakati wa mwisho kupambana na raia. Tunajua, ‘anapotezea’ ili kuvuta muda ili kuwaadalia mazingira wadau wake ili itakapofika wakati aseme; ‘tumeelemewa na nguvu ya umma’ na sasa wajibu wetu ni ‘kuwasindikiza’ ili wakadai watakacho. (3) Mheshimiwa Rais, huyu IGP Ernest Mangu tangu alipoingia madarakani aliingia na sera ya kulivuruga Jeshi la Polisi, kwa kuvunja umoja wa Jeshi uliokuwa umejengwa na watangulizi wake. Jambo hilo, limesababisha kila mmoja (asiyekuwa msingida au kabila lake) ndani ya Jeshi kujiweka kando na hivyo kuwaachia wasingida wenzake. Maana vipaumbele vikuu vya mpango wake wa kazi alioingia nao ni ukabila, kusimamia maslahi yake ya kifedha/rushwa, kuwachafua viongozi waliomlea ili kuwanyog’onyesha kiutendaji, na mradi wa kuwarahisishia wadau wake kufikia malengo yao ya kisiasa. Katika kuyatenda hayo hana muhali, aibu, woga au subira hata kama anajua kwamba ayafanyayo yatajulikana ama yataleta madhara na hasara kubwa kwa taifa. Mheshimiwa Rais, kwa mwenendo huo wa hayo machache tuliyokujulisha, tunapenda ufahamu kwamba Jeshi la Polisi zima (lote) linayumba mno tangu liwe chini ya uongozi wa IGP. Ernest Mangu. Mtu huyu hana sera, wala hana mbinu ama mkakati wowote wa kiutendaji zaidi ya kusimamia hayo mambo yake ya kulivuruga Jeshi. Ndiyo maana tunaomba uelewe kwamba kulingana na Police General Order (PGO), mila na tamaduni za mfumo wa uendeshaji wa Jeshi letu, mwenye akili ni yule aliye juu na kwa kuwa juu umeweka muhaini/muasi, hata kama tulio chini tunajua la kufanya ni vigumu kufanya lolote kwa sababu aaminiki/hatumwamini na mwenye Jeshi ni yeye. Hivyo, katika hali hiyo tegemea kuvuna vituko na aibu itakayoambatana na matokeo ya utendaji ambao utakuacha umeduwaa na huzuni nyingi. Mheshimiwa Rais, kwa ujumla wetu (maofisa na askari wote wa Jeshi la Polisi Tanzania – isipokuwa wasingida na wanyatulu), tunaamini hujachelewa kufanya maamuzi na tunakuomba usiusukume mzigo wa aibu hii na wajibu huu kwa mwingine, wala kusubiri hayo tuliyokudokeza kutokea labda kama ‘ndio mpango wako’ na ‘ndivyo unavyataka iwe!’. Kwa hali ilivyo na jinsi matendo yake ya uasi yalivyotuchosha, tunakuandikia barua hii tukiwa tumejiridhisha kwamba tuko tayari kuweka rekodi ya kujisimamia wenyewe na kufanya kazi kwa juhudi, weledi na bidii kubwa (bila kuwa na IGP muasi) ili kuhakikisha unamaliza salama kipindi chako cha uongozi na Serikali mpya inaanza kazi nchi ikiwa shwari. Ndiyo sababu tunataka ujue kwamba kwa jinsi ulivyotujali, kutuhudumia na heshima uliyotupa tuko tayari kwa kazi ya usiku na mchana bila kiongozi muasi. Vinginevyo ukikaa kimya tutajua na kuamini kwamba umelitosa Jeshi la Polisi zima nyakati hizi za mwisho na, ‘umeamua/umechagua kuvuna mabua maana unacheka cheka na nyani’. Pia, tutaamini kwamba umeyapa kisongo mema yote na juhudi zote ulizozifanya kuliwezesha na kulijenga Jeshi la Polisi tangu ulipoingia madarakani. Hivyo, kwa heshima na unyeyekevu mkubwa tunaomba upokee maoni na ushauri wetu huu uliotokana na uzalendo kwa nchi yetu na uaminifu wetu kwako. Tunatumaini utasikia kilio chetu na kwa maslahi mapana ya taifa na kwa maendeleo na ustawi wa Jeshi letu la Polisi, utakubali kufanya kile ambacho tunakitegemea kutoka kwako mapema, ili kuinua ari na moyo wa utendaji wetu hasa katika kipindi hiki. Afande, Mheshimiwa Rais, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, tunawasilisha tafadhali kwa hatua zako muhimu. Ni sisi maofisa na askari wa Jeshi la Polisi, tulio waaminifu na watiifu kwa mujibu wa kiapo chetu. Nakala:- 1. Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu – Dar es salaam. – Kwa taarifa na hatua sitahiki 2. Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dar es salaam. – Kwa taarifa, kwa sababu yote tuliyoyaandika katika barua hii unayajua. 3. Kwa Vyombo vyote vya habari – Ujulisheni umma.